Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 05:36

Viongozi wa mataifa ya G7 wakubaliana kupiga marufuku uagizaji wa dhahabu kutoka Rashia


Rais Joe Biden akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na viongozi wenzake wa G7.
Rais Joe Biden akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na viongozi wenzake wa G7.

Viongozi wa mataifa 7 tajiri duniani, G7, wameanza mazungumzo ya kuiwekea Rashia vikwazo vipya ili kuibana zaidi kutokana na uvamizi wake wa Ukraine.

Kansela Olaf Scholz, aliwakaribisha viongozi wenzake kutoka Canada, Marekani, Japan, Ufaransa, Utaliana na Uhispania kwenye Kasri ya Elmau, kwenye milima ya Bavaria kwa mazungumzo ya siku tatu kabla ya kuelekea Madrid, Uhispania kwa mazungumzo na wenzao wa ushirika wa NATO.

Wakuu hao wanajaribu kutanzua tofauti zilizopo kati yao kuhusu uvamizi wa Rashia nchini Ukraine huku wakikabiliana na atahri zinazoongezeka duniani kutokana na uvamizi huo.

Rais Biden amemuambia Kansel;a Scholz kwamba"ni lazima tuwe pamojakumonesha Rais wa Rashia kwamba NATO na G7 ziko pamoja na hazijatengana kama alivyotarajia."

Scholz pia amesifu umoja wa nchi za magharibi ambao anasema, "Putin hakutarajia."

Matamshi hayo yametolewa wakati Rashia ilianza tena mashambulizi yake kati kati ya mji mkuu wa Ukraine, wa Kyiv kwa mara ya kwanza Jumapili baada ya muda wa wiki tatu, mashambulio ambayo Biden amelaani akisema "ni ukatili unaoongezeka."

Viongozi wa G7 wanakabiliwa pia na kitisho kinachoongezeka cha kuduma kwa uchumi na kishinikizo cha kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

XS
SM
MD
LG