Kuna historia ndefu baina ya nchi hizo mbili ya uhusiano ulioathiriwa na majeraha ya zamani kutokana na uvamizi wa kikatili wa Japan katika peninsula katika nusu ya kwanza ya karne ya 20.
Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, atakutana na Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kushida, Alhamisi katika siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili ya Rais Yoon nchini Japan.
Itakuwa ni ziara ya kwanza rasmi nchini Japan kwa rais wa Korea Kusini, tangu 2011.
Ziara hiyo inajiri siku chache baada ya serikali ya Yoon kutangaza mpango wa kukusanya fedha za kiraia ili kuwafidia Wakorea ambao walipata fidia kutoka kwa makampuni ya Japan ambayo yaliwafanya watumwa wakati wa uvamizi wa Japan katika Peninsula ya Korea kuanzia 1910 hadi 1945.