Javaid Rehman, mtaalamu huru na maalum wa Umoja wa Mataifa wa hali ya haki Iran, amesema lazime kuwe na uwajibikaji kwa ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu, bila kujali lini ulifanyika.
“Utawala wa Iran na viongozi wake hawapaswi kuruhusiwa kuepuka matokeo ya uhalifu wao dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari,” aliongeza.
Mtaalamu huyo ambaye mamlaka yake yatakamilika Julai 31, amesema katika taarifa yake kwamba uhalifu wa ukatili wa mauaji ya kiholela nje ya mahakama ya 1981 na 1982 pamoja na 1988 yalitokana na uhalifu dhidi ya ubinadamu wa mauaji na yale ya kimbari.
Forum