Mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Maendeleo ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika IGAD, umemalizika Jumanne, bila ya kuweza kupatikana makubaliano kati ya viongozi wa Sudan ya Kaskazini na Kusini juu ya matatizo muhimu yanayotishia kura ya maoni.
Viongozi kutoka mataifa matano wanachama wa IGAD walitoa taarifa ya kuwahimiza viongozi wa Sudan ya kusini na kaskazini kutanzua kwa haraka kabisa tofauti zilizopo kati yao, ikiwa ni pamoja na kupanga kura ya maoni tofauti juu ya ikiwa eneo lenye utajiri wa mafuuta la Abyei lijiunge na kaskazini au kusini, pindi kusini itakapo jiamulia inataka uhuru wake.
Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano huo wa Addis Abeba, balozi wa Kenya nchini Ethopia Monica Juma alisema inaonekana kana kwamba makubaliano juu ya Abyei huwenda yakafikiwa karibuni chini ya uwongozi wa tume maalum ya Umoja wa Afrika inayo ongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.