Viongozi na wakuu wa serikali wa mataifa 19 wanachama wa soko la pamoja la Afrika ya Mashariki, na Kusini COMESA wameanza mkutano wa siku tatu katika mji mkuu wa Swaziland, Mbabane.
Kauli mbiyo ya mkutano ni, "Kuhamasisha Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya Maendeleo", ambapo viongozi wanajadili juu ya maendeleo ya juhudi za kunganisha pamoja shughuli za soko, ikiwa ni pamoja na manedeleo ya kutekeleza kwa ukamilifu Umoja wa Forodha wa COMESA.
Mkutano utajadili pia juu ya ushirikiano kati ya jumia tatu kuu za kanda hiyo, COMESA, Jumuia ya Afrika Mashariki na Jumuia ya Manedeleo ya Kusini mwa Africa SADC, na jinsi kanda hiyo inavyo weza kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia kwa maslahi ya wananchi wao.
Mataifa 19 ya COMESA yana kwa ujumla wakazi milioni 389 wenye kuagizia bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 32 kila mwaka na kusafirisha bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 82.
Wakati wa mkutano huko Rais Robert Mugabe atamkabidhi uwenyekiti wa jumuia hiyo kwa Mfalme Mswati wa tatu.