Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:41

UM: Wanawake bado waathirika wakubwa wa madawa


Alvaro Rodriguez
Alvaro Rodriguez

Utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la idadi ya wanawake na wasichana wanaokamatwa wakijihusisha na makosa ya jinai yanayohusiana na madawa ya kulevya duniani.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez amesema jamii ni lazima iondokane na unyanyapaaji wa wanawake wanaotumia madawa na badala yake wawasaidie kuweza kufikia huduma za matibabu na kuwasaidia kubadilika.

Hafla hiyo ya uzinduzi wa ripoti hio ilihudhuriwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siyanga.

Ripoti inaeleza kuwa thuluthi moja ya watumiaji wa dawa za kulevya duniani ni wanawake na wasichana, ikiwa ni ishara kuwa kati ya kila watu watano wanaopata matibabu kwa kuathirika na madawa ya kulevya mmoja ni mwanamke.

“Naipongeza serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua hii muhimu kupambana na usafirishaji wa madawa na utumiaji haramu wa madawa kinyume cha sheria. Juhudi hizi pia zimesaidia kuongeza mwamko kati ya jamii ya Watanzania juu ya hatari za matumizi mabaya ya madawa,” amesema Mratibu huyo wa UM.

Wakati huo huo washukiwa wakuu watano wa biashara ya madawa ya kulevya wanahojiwa na DCEA ili kutafuta mtandao wao wa biashara hiyo nchini Tanzania na sehemu nyingine duniani.

Kamishna wa Inteligensia wa DCEA Fredrick Kibuta amesema Jumatatu akiwa Dar es Salaam kwamba kwa vile serikali imeanzisha operesheni ya kuwasaka wanaojihusisha na madawa ya kulevya baada ya kuteuliwa Kamishna Mkuu na makamishna wawili wasaidizi; intelijensia na operations, vita dhidi ya madawa ya kulevya imeongeza kasi, na kuelekea katika lengo lililo sahihi.

“Tunawashikilia watu watano ambao ni wanashukiwa, na inadaiwa ni vinara wa biashara ya madawa… hivi sasa wanahojiwa na kwa wakati huu hatuwezi kutangaza majina yao kwa sababu inaweza kuvuruga uchunguzi wetu,” Kibuta amesema wakati wa kuzindua Ripoti ya Bodi ya Kimataifa ya Kuzuia Madawa ya Kulevya ya 2016.

XS
SM
MD
LG