Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:44

Vikwazo wanavyopitia wasichana Tanzania wanaotaka kurudi shule baada ya kujifungua


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtitu, iliyoko mje ya jiji la Dar es Salaam wakati wa mapumziko.Picha na TONY KARUMBA / AFP.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtitu, iliyoko mje ya jiji la Dar es Salaam wakati wa mapumziko.Picha na TONY KARUMBA / AFP.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, msichana mmoja kati ya wanne walio na umri wa miaka 15 mpaka 19 nchini Tanzania ama ni mja mzito au amejifungua.

Sera ambazo ziliwalazimsha kina mama vijana kuacha shule ziliondolewa mwaka 2021. Lakini licha ya kanuni hizi kuondolewa, wengi bado wanashindwa kuwa mama na pia kusoma kwa wakati mmoja.

Neema Kisimakisili ni miongoni mwa wasichana hao, wakati alipopata uja uzito akiwa na umri wa miaka 15, wazazi wake hakufurahishwa na hilo, ndugu zake na jamii pia hawakupendezwa. Licha ya ya changamoto hizo, alihudhuria masomo katika shule binafsi ambayo inashirikiana na serikali kuwasaidia kina mama wasichana kuendelea na masomo yao.

Hata hivyo Kisimakisili, anasema miongoni mwa changamoto anazopitia ni kuwa hana mtu wa kumsaidia kumuangalia mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja wakati akiwa darasani, hivyo anaishi na mtoto wake katika eneo la shule.

Nchini Tanzania baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali na kidini zinatoa huduma ya kuwatunza watoto, lakini mara nyingi hazitoshi kukidhi mahitaji ya kina mama ambao ni vijana, hivyo, huduma za watoto mara nyingi hunaachiwa wazazi vijana au walezi, anasema Esther Manyanda, ambaye ni meneja katika Shule ya chekechea na msingi ya Glad mjini Dodoma.

Mwaka 2021, serikali ya Tanzania iliondoa marufuku ambayo iliwazuia kina mama vijana na wasichana waja wazito kuhudhuria masomo. Matokeo yake, kina mama vijana na wanafunzi wajawazito walirejea shule, zaidi ya 1,600 mwaka 2023 pekee, kwa mujibu wa Wizara ya Elimu.

Serikali inajaribu kufanya mengi zaidi….kushirikiana na taasisi binafsi kupunguza mzigo unaowakabili kina mama vijana ambao hawana huduma ya kusaidiwa ulezi wa watoto. Hii inajumuisha majengo ya mabweni na kutoa elimu ya ngono na chakula cha bure.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa katika hotuba yake bungeni mwezi Mei mwaka huu, alisema serikali ilikuwa ikitathmini sera zake za elimu na kuwa na kanuni ili kushughulikia vyema jinsi wanafunzi hao ambao masomo yao yamekatizwa kwa uja uzito wanavyoweza kurejea shule.

Lakini unyanyapaa bado unaendelea, mjukuu wa Mbua Kitu, Eneza, ambaye ametoa jina lake la kwanza tu kwasababu ya kujificha, alipata uja uzito akiwa na umri wa miaka 15 mwaka 2022. Ingawaje alikuwa na hamu kubwa ya kurejea shule lakini baada ya kujifungua hakuweza kufanya hivyo kutokana na vikwazo mbalimbali.

Eneza hayuko peke yake, ni miongoni mwa vijana ambao wanataka kurejea shule kuendelea na masomo, lakini wanakabiliwa na vikwazo kama vile umaskini, kutengwa na kijamii, na kukataliwa, pamoja na ukosefu wa huduma za watoto. Neema Kisimakisili ana matumaini kuwa siku moja mimba hazitakuwa vikwazo kuwazuia kina mama vijana kutoendelea na masomo yao.

Forum

XS
SM
MD
LG