Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:29

Vikosi vya usalama vya Uganda vimewakamata watu 40

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayejulikana pia kama Bobi Wine, baada ya mkutano wake na waandishi wa habari nyumbani kwake Magere, Uganda, Januari 26, 2021.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayejulikana pia kama Bobi Wine, baada ya mkutano wake na waandishi wa habari nyumbani kwake Magere, Uganda, Januari 26, 2021.

Waandamanaji hao 40 walikamatwa katika mji mkuu wa Kampala na maeneo mengine huku mamlaka ikizuia mipango ya kuandaa kile ambacho upinzani ulisema kuwa ni maandamano ya watu milioni moja siku ya Alhamisi.

Vikosi vya usalama vya Uganda vimewakamata watu 40 wakati wa operesheni dhidi ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani Richard Kyagulani maarufu kama Bobi Wine, ambaye kuwekwa kwake katika kifungo cha nyumbani Marekani imesema kunaonyesha ukandamizaji wa demokrasia katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Waandamanaji hao 40 walikamatwa katika mji mkuu wa Kampala na maeneo mengine huku mamlaka ikizuia mipango ya kuandaa kile ambacho upinzani ulisema kuwa ni maandamano ya watu milioni moja siku ya Alhamisi.

Maandamano hayo yalipaswa kuanza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, kusini mwa mji mkuu, ambako kiongozi huyo Robert Kyagulanyi aliwasili kutoka nje ya nchi.

Polisi waliwakamata washukiwa 40 akiwemo mbunge mmoja kwa kuchochea ghasia, walisema katika taarifa yao siku ya Ijumaa.

Forum

XS
SM
MD
LG