Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 12:50

Vikosi vya serikali ya Somalia vyamaliza uvamizi wa al-Shabab dhidi ya ofisi ya Meya wa Mogadishu


Maafisa wa usalama wa Somalia wakisimama nje ya ofisi ya Meya wa Mogadishu iliyoshambuliwa na Al-Shabab, Januari 22, 2023. Picha ya Reuters
Maafisa wa usalama wa Somalia wakisimama nje ya ofisi ya Meya wa Mogadishu iliyoshambuliwa na Al-Shabab, Januari 22, 2023. Picha ya Reuters

Vikosi vya serikali ya Somalia vimemaliza uvamizi wa zaidi ya saa tano wa jengo lenye ofisi ya Meya wa Mogadishu na vituo vingine vya serikali ya wilaya.

Wizara ya habari, utamaduni na utalii imesema maafisa wa usalama viliwaua wapiganaji sita wa Al-Shabab waliohusika katika shambulio hilo la Jumapili.

Raia watano waliuawa pia na wengine wanne kujeruhiwa, taarifa ya wizara hiyo imeongeza.

Serikali ya Somalia imesema washambuliaji wa al-Shabab walifika kwenye jengo hilo kwa mguu, wakijifanya askari wa serikali.

Shambulio hilo lilianza na mlipuko uliofuatwa na uvamizi wa jengo hilo uliofanywa na watu wenye silaha.

“Majira ya saa sita mchana, walishambulia kwa bomu lango la nyuma lililo mbele ya wilaya ya Hamarweyne,” Naibu Meya Isse Gure amesema.

Gure ameiambia VOA kwamba maafisa wa serikali ya wilaya isipokuwa Meya Yusuf Hussein Jimale walikuwa kwenye jengo hilo wakati shambulio lilipotokea. Jimale yuko nje ya nchi.

XS
SM
MD
LG