Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 06:13

Vijana wanabidi kufahamu ikiwa wameambukizwa na virusi vya HIV au la


Kijana wa Afrika Kusini akipata ushauri nasaha juu ya namna ya kupambana na u nyanyapaa.
Kijana wa Afrika Kusini akipata ushauri nasaha juu ya namna ya kupambana na u nyanyapaa.
Kufuatana na takwimu za idara ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Ukimwi UNAIDS, kati ya watu milioni 35 waloambukizwa na virusi vinavyosababisha ukimwi milioni 25 wanapatikana katika nchi za Afrika kusini mwa janga la Sahara.

Na kiwango cha wanaoishi na virusi vya HIV na wale wenye ukimwi inatofautiana, sawa na tofauti zilizopo kati ya viongozi wa bara hilo kuhusiana na muelekeo wa kupambana nao alieleza mkurugenzi wa masuala ya afya ya taasii inayojulikana One Bw. Erin Hohlfelder.

Katika ripoti iliyotolewa na taasisi ya ONE , kuna nchi 16 za Afrika ambazo waatalamu wanaeleza zimefikia kiwango cha kugeuza mkondo kuelekea kutokomeza ugonjwa huo. Nchi zinazoongoza katika orodha hiyo ni Ghana Malawi na Zambia huku Cameroon, Nigeria na Togo Ziko mwisho ya orodha hiyo
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:19 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kwa upande mwengine Shirika la Afya Duniani WHO linaeleza kwamba licha ya maendeleo hayo ya Afriika ni asili mia 10 ya wanaume vijana na asili mia15 wanawake vijana wanaojua ikiwa wana virusi vya HIV au la.

Ripoti ya WHO iliyotolewa Jumatatu Novemba 25 2013, inaeleza kwamba kuna zaidi ya watoto milioni mbili wadogo kati ya umri wa miaka 10 hadi 19 wanaoishi na HIV kote duniani na miongoni mwa idadi hiyo asili mia 70 ya vijana wanaoishi Afrika.

Ripoti inaeleza kwamba ingawa idadi ya wanaofariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi imepunguka kwa asili mia 30 lakini miongoni mwa vijana imeongezeka kwa asili mia 50.

Craig McClure mkuu wa kitengo cha HIV ukimwi cha Idara ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Watoto UNICEF, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba, kuna haja ya watu kuwa waangalifu zaidi katiika masuala ya vijana wadogo inapohusiana na kupima HIV na kutoa matibabu.

"Katika miaka ya hivi karibuni watu wamekuwa wakizingatia juu ya kuongeza kupima akina mama wajawazito, kuwapatia matibabu ili kulinda afya yao binafsi na kuzuia kuwaambukiza watoto wao wachanga. Sasa tunahitaji kupanua juhudi hizo na kuwapima vijana wadogo ili kuhakikisha kwamba watoto wanabaki katika hali ya kutokua na virusi vya ukimwi tangu wanapozaliwa hadi utuuzima wao. Na wale watoto wenye HIV wanapewa matibabu", amesema McClure.
Idadi ya vifo kutokana na Ukimwi kote duniani , 2001-2012
Idadi ya vifo kutokana na Ukimwi kote duniani , 2001-2012

McClure anasema hatua ya kwanza kuchukuliwa ni kuhakikisha vijana zaidi wanajua hali yao. Katika nchi nyingi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, sheria inamzuia mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 kupimwa HIV bila ya ruhusa kutoka kwa wazazi wao.

"Bila shaka tungelipenda watoto wadogo na vijana kuweza kujadiliana na wazazi wao juu ya mahitaji yao ya afya, lakini tunafahamu hilo silo jambo linalofanyika sana. Kwa hivyo kurahisisha vijana kujipima ikiwa kupitia jamii au vituo vya afya ndiyo njia muhimu kuhakikisha ikiwa wanahitaji huduma za tiba au kujikinga", amwesema McClure.

Ili kuwasaidia vijana ambao wanaishi na HIV au wako hatarini kuambukizwa wanapata huduma wanaohitaji, WHO imefanya kazi na UNICEF na washirika wengine kubuni muongozo wa kupima HIV na huduma maalum kwa vijana wadogo.

Ripoti inatoa wito kwa serikali zote kuwa waangalifu inapohusiana na vijana wadogo katika miradi yao ya HIV na kutathmini sera zinazohusiana na umri wa mtu kupata idhini kutoka kwa wazazi wake.
XS
SM
MD
LG