Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:52

Vifo zaidi Gaza kutokana na mashambulizi ya Israel


Hospitali ya Al-Aqsa, Deir el-Balah katikati mwa ukanda wa Gaza, Nov 9, 2024,
Hospitali ya Al-Aqsa, Deir el-Balah katikati mwa ukanda wa Gaza, Nov 9, 2024,

Idara ya ulinzi wa kiraia katika Gaza imesema kwamba shambulizi la anga la Israel limewaua wapalestina 14 wakiwemo wanawake na watoto, huku jeshi la Israel likisema kwamba lilikuwa limeua darzeni ya wanamgambo kaskazini mwa sehemu hiyo.

Msemaji wa idara ya ulinzi wa kiraia Mhamud Bassal ameliambia shirika la habari la AFP kwamba shambulizi la anga lilipiga hema la wakimbizi wa Palestina huko Khan Yunis, kusini mwa Gaza, na kuua watu tisa, wakiwemo watoto na wanawake.

Shirika la msaada la Red Crescent la Palestina, limethibitisha vifo hivyo, na kusema kwamba watu wengine 11 walijeruhiwa katika shambulizi hilo na wamepelekwa katika hospitali ya Nasser.

Shambulizi la pili la anga limeua watu 5 wakiwemo watoto na kujeruhi watu wengine 22, ndege za kijeshi za Israel zilipopiga shule ya Fahad Al-Sabah, ambako maelfu ya watu waliokoseshwa makazi wanaishi, katika wilaya ya Al-Tuffah, ya Gaza City.

Waliofariki au kujeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya Al-Ahli Arab.

Forum

XS
SM
MD
LG