Makundi ya wahalifu yamevamia Haiti katika wiki za hivi karibuni kushambulia taasisi muhimu na kufunga uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa. Machafuko hayo yamewasukuma raia wengi wa Haiti kwenye ukingo wa njaa, na kuwaacha wengi zaidi katika hali ya kukata tamaa.
UNICEF ilisema kuwa kontena la usafirishaji lililojaa vifaa muhimu vya msaada limeporwa huku serikali ya Guatemala ikisema kuwa kituo cha ubalozi pia kiliibiwa.
Marekani ilikuwa imepeleka kwa ndege vikosi vya kijeshi ili kuimarisha usalama katika Ubalozi wake, na pia kufanya kile kilichoonekana kama kukanusha uvumi kwamba maafisa wakuu wa serikali ya Marekani wanaweza kuondoka nchini humo.
Forum