Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:10

Vatican yathibitisha kuwa Papa Francis ataongoza ibada ya mkesha wa Pasaka Jumamosi usiku


Papa Francis akiongoza sala ya Malaika wa Bwana kutoka dirishani kwake Vatican
Papa Francis akiongoza sala ya Malaika wa Bwana kutoka dirishani kwake Vatican

Vatican ilithibitisha kuwa Papa Francis ataongoza ibada ya mkesha wa Pasaka Jumamosi usiku, baada ya kuamua dakika za mwisho kutoshiriki   katika maandamano ya Ijumaa Kuu katika ukumbi wa Colosseum kama tahadhari ya afya.

Taarifa ya kila siku ya Vatikani ilithibitisha kwamba Francis ataongoza mkesha huo mrefu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, moja ya matukio muhimu katika kalenda ya kiliturujia ya kanisa katoliki. Ibada hiyo inayotarajiwa kuanza saa moja na nusu usiku na kwa kawaida huchukua muda wa saa mbili, kuadhimisha ufufuko wa Yesu na inajumuisha sakramenti ya ubatizo kwa watu wazima wanane waliojiunga na kanisa hilo.

Francis mwenye umri wa miaka 87, ambaye sehemu ya pafu lake moja ilitolewa alipokuwa kijana, amekuwa akipambana na matatizo ya kupumua wakati wote wa majira ya baridi ambayo yamemfanya kuwa vigumu kwake kuzungumza kwa muda mrefu.

Forum

XS
SM
MD
LG