Makundi manne yamesitisha uzalishaji wa mafuta kote Libya.
Waandamanaji wanamtaka Waziri mkuu wa Tripoli Abdul Hamid Dbeibah kukabidhi madaraka kwa serikali hasimu inayoongozwa na Fathi Bashaga, iliyoundwa mwezi uliopita.
Serikali hizo mbili zimekuwa zikishindana kuchukua madaraka tangu bunge la Libya lilipomteua Bashaga kuwa Waziri mkuu.
Lakini Dbeibah amesema kwamba bado ana mamlaka ya kuongoza taifa hilo hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika mwezi June.