Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuondoka Uturuki kuelekea Uzbekistan kwa kongamano na Turkic, Erdogan hata hivyo hajasema iwapo hatua hiyo itapelekea kufanyika mazungumzo kati ya Russia na Ukraine, lakini amesema Uturuki inaendelea na juhudi za kufanyika mazungumzo.
"Kazi ya upatanishi inaendelea bila matatizo lakini sio jambo la busara kusema tarehe maalum na wakati juhudi za upatanishi zitafanikiwa au kumalizika," amesema Edrogan
Moscow imeamurisha wanajeshi wake kuondoka sehemu ambazo wamekuwa wakishikilia katika ukingo wa magharibi wa mto Dnipro, ikiwemo mji mkuu wa Kherson.
Wanajeshi wa Russia wamekuwa wakishikilia Kherson tangu walipovamia Ukraine mwezi Februari.
Ukraine imeonya kwamba Russia imeondoka Kherson kimkakati, na huenda ikapelekea mji huo kuwa na mapambano mabaya zaidi yatakayopelekea vifo na uharibifu mkubwa, na kuufanya kuwa mji wa mauti.
Mkuu wa jeshi la Ukraine hajathibitisha iwapo kweli wanajeshi wa Russia wanaondoka Kherson, lakini amesema kwamba wanajeshi wa Ukraine wamesonga mbele kilomita saba katika muda was aa 24 na kudhibithi sehemu 12.
Russia imesema kwamba wanajeshi wake wanaelekea katika sehemu za upande wa kushoto wa mto Dnipro kulingana na mpango wao ulioidhinishwa, huku wanajeshi wa Ukraine wakiendelea kudhibithi sehemu kadhaa za kusini mwa Ukraine.