Uchaguzi utafanyika kesho Jumapili, katika nchi hiyo yenye changamoto nyingi kuhusu maswala yake ya ndani.
Erdogan, mwenye umri wa miaka 69, amejipa madaraka makubwa katika muda wa miaka 20 ambayo amekuwa madarakani.
Alimaliza wa kwanza katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika Mei 14 lakini hakupata ushindi wa moja kwa moja licha ya kupata viti vingi vya bunge.
Uturuki inakabiliana na mfumuko mkubwa wa bei na athari za baada ya kutokea tetemeko baya la ardhi lililoua zaidi ya watu 50,000, kusini mwa nchi hiyo.
Erdogan anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Kemal Kilicdaroglu, mwenye umri wa miaka 74, ambaye ni mgombea kwa tiketi ya muungano wa vyama sita vya upinzani.
Ameahidi kubadilisha mfumo wa miaka mingi wa Erdogan, unaoripotiwa kuvuruga demokrasia nchini Uturuki. Ameahidi pia kuwafukuza wakimbizi kutoka Syria na kuimarisha haki za wanawake.
Forum