Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:51

Utawala wa kijeshi Mali utachukua miezi 24 kurejesha utawala wa kiraia


Ujumbe wa upatanishi wa ECOWAS walipokutana na viongozi wa mapinduzi wa Mali.Agosti 22,2022.(REUTERS/Mamadou Keita).
Ujumbe wa upatanishi wa ECOWAS walipokutana na viongozi wa mapinduzi wa Mali.Agosti 22,2022.(REUTERS/Mamadou Keita).

Utawala wa kijeshi wa Mali utachukua miezi 24 kuanzia Machi 2022 kurejesha utawala wa kiraia baada ya mapinduzi ya Agosti 2020, msemaji wake alisema Jumatatu.

Hii ikiwa hatua ya hivi karibuni katika mazungumzo na jumuiya ya kikanda ya ECOWAS kuondoa vikwazo vinavyodumaza uchumi.

Viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi wamekuwa chini ya shinikizo la kurejesha demokrasia tangu walipopindua serikali na kushindwa kutimiza ahadi ya kuandaa uchaguzi mwezi Februari, na kusababisha vikwazo kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).

Muda wa mpito umewekwa kuwa miezi 24, msemaji wa serikali ya mpito Abdoulaye Maiga alisema kwenye televisheni ya kitaifa, na tarehe ya kuanza ikiwa Machi 26, 2022.

XS
SM
MD
LG