Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:54

Utawala wa jeshi wa Guinea watangaza kuvunja serikali


Viongozi wa kijeshi wa Guinea. Picha ya maktaba.
Viongozi wa kijeshi wa Guinea. Picha ya maktaba.

Viongozi wa kijeshi nchini Guinea wametangaza kuvunja serikali bila kutoa maelezo, waksiema watateua serikali mpya,  katibu mkuu wa rais amesema.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP Jenerali Amara Camara kupitia ujumbe wa video Jumatatu usiku amesema kwamba shughuli za kila siku zitaendelea kama kawaida chini ya manaibu makatibu wakuu, hadi pale serikali mpya itakapo undwa.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limekuwa likiongozwa na jeshi tangu wanajeshi walipoipindua serikali ya Rais Alpha Conde 2021. Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, imesukuma kurejeshwa kwa utawala wa kiraia, wakati uchaguzi mkuu ukipangwa kufanyika 2025.

Mkuu wa majeshi Sory Bangoura amesema Jumatatu kwamba maafisa wa serikali iliyovunjwa wanatakiwa kurejesha magari ya serikali pamoja na hati za kusafiria haraka iwezekanavyo. Walinzi wao pia wamesitisha huduma zao, wakati akaunti za mawaziri kwenye benki zimezuiliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG