Utawala wa Biden unaunda mchakato mpya unaolenga kupunguza muda kuamua hatima ya wahamiaji wapya waliowasili katika mahakama za uhamiaji kutoka miaka kadhaa hadi takriban miezi sita wakati ambapo uhamiaji unaongeza wasiwasi miongoni mwa wapiga kura.
Chini ya mpango huo uliotangazwa Alhamisi, wahamiaji watu wazima ambao wameingia nchini peke yao na wanakwenda katika miji mitano maalum kesi zao zinasimamiwa na kundi la majaji kwa lengo la kuwafanya watoe uamuzi ndani ya siku 180.
Hiyo itaashiria mabadiliko ya haraka zaidi kuliko kesi nyingi zilizo katika mfumo wa uhamiaji nchini, ambao unaweza kuchukua wastani wa miaka minne kutoka mwanzo hadi mwisho. Na kwa kuamua kesi haraka, mamlaka zinaweza kuwaondoa kwa haraka zaidi watu ambao hawastahili kukaa nchini.
Lakini haijulikani ni wahamiaji wangapi watapitia utaratibu huu mpya, na kuibua maswali kuhusu jinsi utakavyokuwa na ufanisi. Maelezo hayo yalitolewa na maafisa waandamizi wa utawala wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari siku ya Alhamisi. Walizungumza kwa masharti ya kutotajwa kulingana na miongozo iliyowekwa na utawala.
Forum