Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:42

Usitishaji mapigano Syria bado ni kitendawili


Wapiganaji wa Kurdish People's Protection Units-YPG
Wapiganaji wa Kurdish People's Protection Units-YPG

Mkuu wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa, Mark Lowcock alisema Jumatano kwamba mpango wa kusitisha mapigano kwa siku 30 kote Syria haujatekelezwa na analiuliza baraza la usalama lini zoezi hilo litatekelezwa. Baraza hilo kwa kauli moja lilipitisha azimio siku ya Jumamosi likitaka mapigano yasitishwe kwa mwezi mmoja ili kuruhusu msaada kuingia ndani ya kitongoji cha Damauscus cha Ghuta mashariki na kuwatowa wagonjwa mahututi pamoja na waliojeruhiwa.

Mark Lowcock aliuliza kama hakujakuwepo na nafasi ya kuwasilisha msaada wa dharura tangu azimio lipitishwe jumamosi, basi nini kimetokea katika siku chache zilizopita? Aliendelea kusema kwamba kuongezeka kwa mashambulio ya mabomu, mapambano, uharibifu mkubwa, kusababisha wanawake na watoto kuwa vilema, njaa zaidi, mahangaiko zaidi na mengineyo.

Mkuu wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa, Mark Lowcock
Mkuu wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa, Mark Lowcock

Lowcock alisema Umoja wa Mataifa na washirika wake wapo tayari wakiwa na malori yaliyojaa msaada wa dharura pamoja na mipango ya kuhamisha wagonjwa mara baada ya milio ya bunduki itakapositishwa na kutoa fursa ya kuingia Syria.

Alitaja juu ya ripoti za mashambulizi ya anga yanayofanywa na ndege za serikali zikidondosha mabomu ndani ya mapipa pamoja na mashambulizi ya ardhini kwa kutumia mizinga dhidi ya wilaya ya Ghouta ya mashariki na darzeni ya wilaya nyingine, siku mbili baada ya kuidhinishwa azimio la usitishaji wa mapigano.

Kwa upande mwingine Russia ambayo iliunga mkono azimio hilo imeweka mpango wake wenyewe wa kusitisha mapigano kwa saa tano kila siku ndani na karibu ya Ghouta. Tangu Februari 18 watu 580 wameshauliwa katika eneo hilo na inaripotiwa kwamba roketi zinazofyatuliwa kutoka Ghouta hadi ndani ya Damuscus zimesababisha vifo vya watu 15 na zaidi ya wayu 200 kujeruhiwa.

XS
SM
MD
LG