Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 13:16

Marekani yaelezea wasi wasi na serikali ya Somalia


Rais wa Somalia, Sheikh Sheriff Sheikh Ahmed(L) akiwa na Waziri Mkuu wake Mohamed Abdullahi Mohamed(R) mjini Mogadishu
Rais wa Somalia, Sheikh Sheriff Sheikh Ahmed(L) akiwa na Waziri Mkuu wake Mohamed Abdullahi Mohamed(R) mjini Mogadishu

Marekani imeelezea wasi wasi kuhusu hatua ya serikali ya Somalia kuwazuia dazeni ya wabunge kusafiri nje ya nchi hiyo.

Maafisa wanasema majeshi ya usalama ya Somalia yaliwazuia zaidi ya wabunge 40 kusafiri kuelekea Kenya hapo jana Jumatatu, ambapo walikuwa wazungumzie hali ya baadae kuhusu uchaguzi.

Taarifa ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi iliwashutumu wafanyakazi wa usalama kwa kuwatisha wabunge kwa silaha na kuwashambulia kimwili wabunge watatu kati yao.

Ubalozi ulisema katika wiki za karibuni kuwa serikali ya mpito imechukua hatua kukomesha mazungumzo ya amani ya kisiasa na kunyamazisha ukosoaji wake.

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, amekuwa katika mapambano ya hadharani ya madaraka na spika wa bunge, sharif Hassan sheikh aden.

Viongozi hao wawili na washirika wao hawakubaliani juu ya namna ya kuitisha uchaguzi, na huenda ukatokea ushindani kwa rais wakati wowote uchaguzi utakapofanyika.

XS
SM
MD
LG