Jenerali wa cheo cha juu wa Marekani amesema jeshi la Marekani lipo tayari kutoa msaada zaidi kwa majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Jenerali William Ward, ambaye ni mkuu wa kitengo cha jeshi la Marekani kwa Afrika, amesema Marekani inatumai kutoa mafunzo zaidi, usafiri na msaada wa kiufundi kwa jeshi la Umoja wa Afrika-AMISOM. Ward alitamka hayo Jumanne alipokuwa akihutoa hotuba katika taasisi ya mikakati na mafunzo ya kimataifa mjini Washington.
Marekani kwa sasa inatoa mafunzo na vifaa vingine kwa kikosi cha AMISOM, ambacho kina wanajeshi elfu kadhaa kutoka Uganda na Burundi. Wanajeshi hao huzozana mara kwa mara na waasi wa Somalia, ambao wanajaribu kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia.
Kikosi hicho cha AMISOM kimesaidia serikali hiyo kuweka udhibiti wake katika maeneo muhimu ya mji mkuu wa Mogadishu, kama vile uwanja wa ndege, bandari na kasri ya rais.
Jenerali wa cheo cha juu wa Marekani amesema jeshi la Marekani lipo tayari kutoa msaada zaidi kwa majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.