Takwimu rasmi za serikali zimeonyesha chama hicho chenye msimamo wa kati kushoto kikiongoza kwa viti 33 baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 64 ya kura, kando na viti 20 kilichopata kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi, katika bunge hilo lenye jumla ya viti 141.
Chama tawala cha Homeland Union Party, kilipata viti 6 kando na zile 18 kilichopata kwenye duru ya kwanza. Taifa hilo la Baltic lenye jumla ya wakazi milioni 2.9 kina mfumo wa upigaji kura ambapo nusu ya viti vya bunge huchaguliwa kupitia wingi wa kura, huku vilivyobaki vikiwa ni kupitia uchaguzi wa marudio kwenye wilala kati ya wagombea wawili wanaoongoza, na mara nyingi hunufaisha vyama vikubwa.
Iwapo chama cha Social Democrats kitafaulu kuunda serikali, basi kinatarajiwa kuendeleza msimamo wa Lithuania dhidi ya Russia, pamoja na utumizi mkubwa wa fedha za ulinzi. Tiafa hilo mwaka huu litatumia takriban asilimia 3 ya mapato yake ya ndani kwenye jeshi, kulingana na makadirio ya NATO, na kwa hivyo kulifanya kuwa taifa la 6 mwanachama ifikapo kwenye matumizi ya kiusalama.
Forum