Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:24

Upinzani waomba Maduro amalize 'ghasia na mateso' Venezuela


Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro

Kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Jumamosi ameomba rais Nicolas Maduro kumaliza ‘ghasia na mateso,’ saa chache baada ya mahakama kusema kuwa uamuzi wake unaotarajiwa kuhusu utata wa uchaguzi wa Julai 28 hauwezi kukatiwa rufaa.

Edmundo Gonzalez Urrutia ambaye anadai kushinda kwenye uchaguzi huo kwa kura nyingi, kupitia ujumbe alioweka kwenye mitandao ya kijamii ameomba Maduro aruhusu uhuru wa kujieleza kisiasa. Hilo ni kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi huo, na kupelekea watu 24 kufa, huku wengine 2,200 wakikamatwa.

“Kuitisha kuheshimiwa kwa katiba yetu sio hatia, kuandamana kwa amani ili kulinda uamuzi wa mamilioni ya watu wa Venezuela siyo hatia pai,” amesema Urrutia mwenye umri wa wa miaka 74, na ambaye ni mwanadiplomasia wa muda mrefu. Ujumbe huo umekuja baada mwanasisa huyo kutoonekana hadharani kwa zaidi ya wiki moja, kufuatia taarifa kutoka mahakama ya Juu, kwamba uamuzi unaosubiriwa kuhusu matokeo ya uchaguzi huo hauwezi kukatiwa rufaa.

Hata hivyo baadhi ya waangalizi wamesema kuwa mahakama Kuu ni tiifu kwa Maduro, aliedai kushinda kwenye uchaguzi huo kwa kura chache. Viongozi wa upinzani wanadai kuwa Urrutia, alishinda kwa kura nyingi, wakati wakiionyesha kile wanachosema ni matokeo ya kura kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.

Forum

XS
SM
MD
LG