Ikiwa imebaki siku nne kabla ya wapiga kura nchini Uganda kwenda kumchagua rais wao na wabunge, vyama vya upinzani vimetoa wito Jumatatu kuahirishwa kwa Uchaguzi huo.
wagombea kiti cha rais watatu, Olara Otunnu wa chama cha UPC, Dk Abedi Bwanika wa PDP, na Samuel Obega mgombea binafsi, wanaitaka tume ya uchaguzi iahirishe uchaguzi mkuuwa Ijuma wakidai kuwa maandalizi ya utaratibu huo wa uchaguzi hayako tayari.
Kwa upande mwengine ripoti za kuaminika kutoka Kampala zinaeleza kwamba mgombea kiti cha rais wa chama cha UPC Bw. Otunnu amelazwa hospitali kufuatia ajali ya barabarani akitokea mkutano wa kampeni Jumatatu usiku.
Hakuna habari zaidi zinajuliukana kuhusiana na ajali hiyo.