Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:39

Upinzani nchini Kenya wafanya ibada kuwakumbuka waliopoteza maisha na kujeruhiwa katika maandamano

Waunga mkono wa maandamano ya upinzani dhidi ya serikali wakweka maua kwenye ibada ya mkesha kuwakumbuka waandamanaji waliofariki wakati wa maandamano ya kuipinga serikali ya kupinga kuongeza ushuru jijini Nairobi, Kenya.Julai 26. (REUTERS).

Upinzani nchini Kenya siku ya Jumatano ulifanya ibada na kuwasha mishumaa katika miji mikubwa kwa zaidi ya darzeni ya  watu waliopoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa wakati wa maandamano mwezi huu kupinga gharama kubwa ya maisha na nyongeza ya kodi iliyopitishwa mwezi Juni.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametoa wito mara kwa mara wa vitendo vya ukaidi wa raia dhidi ya serikali anayoituhumu kwa kuongeza gharama ya maisha na kujinyakulia mamlaka.

Muungano wa Azimio la Umoja anaouongoza ulifanya maandamano matano mapema mwezi huu na kusababisha usumbufu mkubwa ambao katika baadhi ya matukio uliishia kwa makabiliano makali na polisi.

Polisi waliuwa watu 37 wakati wa maandamano hayo shirika la kutetea haki za binadamu la Independent Medico-Legal Unit lilisema mapema wiki hii huku Azimio la Umoja likidai kuwa takriban watu 50 waliuawa.

Forum

XS
SM
MD
LG