Muungano wa upinzani nchini Kenya, The National Super Alliance, Alhamisi ulitarajiwa kutangaza kiongozi atakayewania urais kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Muungano huo Maarufu kama NASA, ulifanya mkutano wake katika bustani za Uhuru Park, mjini Nairobi, ambapo vinara watano wa muungano huo walitarajiwa kutangaza jina la yule atakayepeperusha bendera yao.
Vinara hao ni kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, kiongozi wa Wiper National Movement, Kalonzo Musyoka, yule wa Ford Kenya, Moses Wetangula, kiongozi wa Amani National Congress, Moses Mudavadi, na yule wa Maendeleo Mashinani, Isaac Ruto.
Hayo yanajiri huku chaguzi za mchujo, kuwatafuta wagombea wa nyadhifa mbali mbali, watakaowakilisha vyama vya kisiasa, zikiendelea kufanyika nchini kote.