Mkuu wa moja kati ya vyama vya upinzani CDP, Anicet Niyongabo wa chama cha CDP amesema "tumepata mualiko wa Mkapa lakini kutokanamwenendo wake, imetusababisha sisi kama wajumbe wa vuguvgu la vyama vya upinzani la CNRED kutokuwa na imani naye, na hivyo hatutakihudhuria kikao hicho."
Akizungumza na Sauti ya Amerika Bw. Niyongabo anasema baadhi ya wakuu wa CNARED wamevitaka vyama venye nia ya kususia mazungumzo ya Arusha kubadili msimamo wao.
Mvutano huu umetokea baada ya Mkapa kusema mwezi Disemba mwaka jana alipotembelea Bujumbura kuwa "utalawa wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ni halali na kwamba wanaodai kuwa hawautambui i wana matatizo ya kiakili."
Hata hivyo msemaji wa chama cha UPRONA Tatien Sibonama kutoka tawi lisilo tambuliwa na serikali amesema ni muhimu kwa vikao vifanyike kama kweli bado wanakubaliana kuhusu umuhimu wa mazungumzo.
Msemaji wa UPRONA aliongezea kusema kwamba "kwa yule ambaye hataki mazungumzo yafanyike, anayetaka nchi ibakie katika hali ya sintofahamu basi ataonekana."
Mkapa ameitisha kikao cha Arusha Jumatatu kwa lengo la kukutana na wadau ambao hakuweza kukutana nao wakati wa ziara yake ya misho huko Burundi, ili kujaribu kufikia makubaliano ya mwisho hapo mwezi Juni mwaka huu.
Lakini ianvyonekana mvutano huo unaweza kuchelewesha mazungumzo ya kufikia mukubaliano yatakayo waruhusu wapinzani, wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na wakimbizi wengine zaidi ya laki mbili na nusu waliokimbia Burundi kurejea makwao na wafungwa wa kisiasa kuachiliwa huru., na hatimae kutanzua suala la mhula wa tatu wa Rais Nkurunziza.