Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:42

Unywaji wa bia utaruhusiwa katika kombe la dunia nchini Qatar


Hammad Al Suwaidi, akiwa amesimama kando ya kombe lake kubwa la kombe la dunia ambalo aliwaagiza wachongaji wa Uturuki kumtengenezea. REUTERS
Hammad Al Suwaidi, akiwa amesimama kando ya kombe lake kubwa la kombe la dunia ambalo aliwaagiza wachongaji wa Uturuki kumtengenezea. REUTERS

Unywaji wa bia utaruhusiwa katika Kombe la Dunia nchini  Qatar mwaka huu kwa mujibu wa mkuu wa mashindano hayo alisisitiza hivi karibuni  licha ya vikwazo vikali vya uuzaji wa pombe katika taifa la Kiislamu la Ghuba.

Unywaji wa bia utaruhusiwa katika Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka huu kwa mujibu wa mkuu wa mashindano hayo alisisitiza hivi karibuni licha ya vikwazo vikali vya uuzaji wa pombe katika taifa la Kiislamu la Ghuba.

Katika Kombe la Dunia, bia itauzwa katika maeneo maalum kuzunguka viwanja nane vya mashindano kabla na baada ya michezo, katika eneo la mashabiki na maeneo maalum.yaliyotengwa

Zikiwa zimebakia chini ya siku 73 hadi Kombe la Dunia la kuanza katika taifa la Kiarabu, mtendaji mkuu Nasser al-Khater alisema kuna ‘dhana potofu’ kuhusu uuzaji wa pombe, na kuitaja kuwa moja ya ukosoaji ‘usio wa haki’ unaoikabili Qatar.

Bei ya malazi na upatikanaji wa bia vimekuwa miongoni mwa masuala makuu yanayowatia wasi wasi mashabiki.

"Kwa ufupi sana, tulisema kila mara kwamba uuzaji wa pombe unapatikana hapa Qatar. Pia tulisema wakati wa Kombe la Dunia tutaifanya ipatikane katika maeneo maalum kwa ajili ya mashabiki," Khater alisema.

“Nadhani kuna dhana potofu kuhusiana na uuzaji wa pombe viwanjani,” aliongeza.

Tunafanya kazi kama Kombe jingine lolote la Dunia ambapo hili ni jambo la kawaida na halina tofauti na Kombe jingine lolote la Dunia.

Ingawa Qatar sio kavu, kama vile mataifa mengine ya Ghuba --Saudi Arabia na Kuwait, pombe inaweza kununuliwa na wakazi katika duka moja tu maalum la serikali na takriban baa katika hoteli na migahawa 35.

Kunywa pombe hadharani kwa kawaida ni kinyume cha sheria. Pia mbali na viwanja vya michezo, na katika hoteli na baa za Doha, itakuwa ‘biashara kama kawaida’ kwa wanywaji, maana pombe ni haram na marufuku.

Nchi nyingi zina vizuizi kwa uuzaji wa bia kwenye hafla za michezo. Kwa mfano katika mechi za Ligi Kuu ya Uingereza, mashabiki hawaruhusiwi kunywa pombe wakiwa uwanjani. Hiyo ilikuja baada ya miaka mingi ya washabiki wa mpira kugombana kwenye majukwaa baada ya kulewa.

XS
SM
MD
LG