Na BMJ Muriithi
Vijimambo ni Makala yanayoangazia baadhi ya habari zisizo za kawaida zililizojiri. Huwa tuankukusanyia maajabu, vituko na sarakasi kutoka pembe tofauti tofauti za ulimwengu.
Baada ya kuupa mkono wa buriani mwaka wa 2015 na huku tukiukaribisha mwaka wa 2016, hebu kwa kifupi tu tuone baadhi ya habari zilizokufanya wewe shabiki wa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kukaa karibu na redio yako bila kubaduka, hususan uliposikia mwaka jana kwamba ulikuwa ni wakati wa Vijimambo.
Januari tulianza na habari za viongozi wawili wa kisiasa huko nchini Kenya, rais uhuru Kenyatta, na waziri mkuu wa zamani na mwenyekiti wa chama cha upinzani cha ODM, Raila Odinga, kutofautiana hadharani kuhusu chai. Uhuru Kenyatta.
SIKILIZA hapa:
Na mwezi februari tulisalia huko huko Afrika mashariki ambako mtu mmoja ambaye alikuwa amekataa kata kata kuoga kwa Zaidi ya miaka 17, alifumaniwa na wananchi walioapa kwamba hawangeweza tena kuvumilia uvundo uliotoka kwa bwana huyo na kuamua kumuosha hadharani. Lakini, baada ya kutakasika, bwana huyo aliwahutubia waandishi wa habari…
Mwezi machi tulikuwa na vituko vingi. Lakini kile kiliwashangaza wengi Zaidi ni kuhusu mtu aliyezikwa pamoja na ng’ombe….
Na stori hiyo haikuwa ya kipekee kwani mnamo mwaka wa 2012, kituo cha televisheni cha radio citizen, kilikuwa kimetangaza kisa kama hicho ambapo ngama alizikwa akiwa hai.
Mwezi wa tatu tulikuletea mengi, baadhi yake ni kuhusu kahaba aliye mzee Zaidi ulimwenguni kukamatwa kwa kufanya ukahaba bila idhini.
Vile vile tulikuwa na habari kutoka hapa Marekani kuhusu watoto wa miaka mitano waliofumaniwa wakifanya mapenzi darasani. Maajabu si haba!
Katika Makala yetu ya leo, vile vile tunakuacha na baadhi ya matamshi ya watu ambao tumewanukuu kwenye vipindi vyetu vya vijimambo vya mwaka wa 2015.
Na kwa hayo msikilizaji tunalikunja jamvi la vijimambo ambapo hii leo tumepiga darubini baadhi ya mengi ambayo tuliwahi kukuletea katika mwaka wa 2015. Kutoka Meza ya Vijimambo, twakutakia mwaka mpya usio na vituko, maajabu wala sarakasi, na badala yake uwe na mwaka wenye mafanikio chungu nzima.
Kama kawaida, nakuacha kwa kauli yetu ya wiki, kwamba asiyejua maana, haambiwa maana. Kisa na maana… dunia imejaa vijimambo! Mimi ni BMJ Muriithi kutoka idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Washington DC.