Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:01

UNHCR yasema mamilioni ya watu wanaathiriwa na mafuriko Afrika Magharibi na Kati


Wakimbizi wa Burundi wakitafuta maji
Wakimbizi wa Burundi wakitafuta maji

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi – UNHCR limesema Ijumaa kwamba mamilioni ya watu wanaathiriwa kutokana na mafuriko huko Afrika Magharibi na Kati,  eneo ambalo limegubikwa na mizozo, ukosefu wa uthabiti na umaskini.

UNHCR imesema kwa zaidi ya miezi miwili mafuriko makubwa yametokea, ambayo kwa baadhi yalikuwa mabaya sana kutokea katika kipindi cha muogo mmoja, na kusababisha watu zaidi ya milioni 3.4 kukoseshwa makazi nchini Nigeria, Chad, Niger, Burkina Faso, Mali na Cameroon.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema kaskazini mashariki mwa Nigeria mafuriko yameathiri takriban watu milioni 3, kuua mamia, na kuwakosesha makazi zaidi ya milioni 1.3. Maji mafuriko, yameosha maeneo ya makazi yaliyokuwa yakihifadhi zaidi ya watu milioni 2 ambao walikimbia mapigano ya wanamgambo wa Boko Haram katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe.

Msemaji wa UNHCR Olga Sarrado alisema Chad ilitangaza hali ya dharura baada ya mafuriko kuwaathiri zaidi ya watu milioni 1 huko. Alisema mito imefurika hadi juu yak ingo zake, mashamba yamefunikwa na maji, mifugo imekufa, na kuwalazimisha zaidi ya watu. 90,000 kukimbia nyumba zao.

“Katika nchi za Sahel ya Kati - Burkina Fasop, Niger, na Mali – mvua kuliko viwango vya wastani na mafuriko yameua mamia ya watu, maelfu kukoseshwa makazi, na takriban hekta milioni 1 mazao zimeoshwa. Hali mbaya sanaz ya hewa katika eneo la Sahel, imechochea ukame na mafuriko, kushusha viwango vya mazao na kuchangia kwa jumla kudorora kwa huduma za umma kwa moja ya mizozo mibaya sana ya ukosefu wa makazi,” amesema Sarrado.

UNHCR imesema makundi yenye silaha yanasambaza vitisho na khofu katika eneo hilo, pamoja na umaskini na ukosefu wa usawa, hali ambayo imepelekea takriban watu milioni 5 katika Sahel kukimbia nyumba zao. Karibu milioni 3 ya hao, shirka hilo limesema, bado wako ndani nchi zao, wakati wengine wamekimbilia katika nchi jirani.

Shirika hilo limesema mzozo wa hali ya hewa unaharibu halli ya maisha, kuvuruga usalama wa chakula, kuzidisha mizoz juu ya uhaba wa rasilimali, na kuwasukuma watu kutoka kwenye nyumba zao.

Sarrado aliomba msaada zaidi kwa wale ambao wako mstari wa mbele katika mzozo wa hali ya hewa ili kuwasaidia kukabiliana na matokeo yake.

XS
SM
MD
LG