Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Julai 05, 2024 Local time: 02:22

UNHCR inaongeza mpango wa misaada wa Sudan ikijumuisha Uganda na Libya


UNHCR- Shirika la Umoja wa mataifa la Kuhudumia Wakimbizi.
UNHCR- Shirika la Umoja wa mataifa la Kuhudumia Wakimbizi.

Sudan tayari ina matatizo ya ukosefu wa makazi duniani ambako watu milioni 12 walilazimika kukimbia vita nchini mwao

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi-UNHCR limesema leo Jumanne kuwa linaongeza mpango wake wa misaada ya Sudan kwenda nchi mbili mpya, Libya na Uganda ambapo idadi ya wahamiaji wanaowasili imeongezeka.

Sudan tayari ina matatizo mabaya sana ya ukosefu wa makazi duniani ambako takriban watu milioni 12 walilazimika kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe na zaidi ya milioni 2 hawana makazi katika upande mwingine wa mipaka. Upanuzi wa hivi karibuni ikiwa ni majibu ya mpango wa Umoja wa Mataifa unafikisha idadi ya mataifa saba ya Afrika yanayopokea idadi kubwa ya wakimbizi wa Sudan.

Kuwasili kwa wakimbizi wa Libya kunaongeza matumaini yao kuwa wakimbizi huenda wakaendelea na safari yao ya kwenda Ulaya, hali ambayo mkuu wa UNHCR tayari ameonya kuwa ni mbaya kama misaada haitatolewa. Waraka wa mpango wa UNHCR uliochapishwa siku ya Jumanne ulionyesha kuwa shirika hilo linatarajia kupokea watu 149,000 nchini Libya kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Ramani ya Uganda na nchi zilizo jirani nazo.
Ramani ya Uganda na nchi zilizo jirani nazo.

Ina miradi 55,000 kwa Uganda ambayo haishiriki moja kwa moja na mpaka wa Sudan. Ewan Watson wa UNHCR aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva, kwamba inajieleza tu na hali ya kukata tamaa na maamuzi ambayo watu wanayafanya, kwamba yanaishia mahali kama Libya ambayo bila shaka ni hali ngumu sana kwa wakimbizi kwa sasa.

Tayari zaidi ya wakimbizi 20,000 waliwasili Libya tangu mwaka jana, na idadi ya wanaowasili imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni na maelfu zaidi ya watu hao hawajasajiliwa Watson aliongeza. Angalau wakimbizi 39,000 wa Sudan waliwasili Uganda tangu vita vilipoanza, Watson alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG