Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:23

Shirika la kimataifa la kazi ILO linabashiri ukosefu wa ajira duniani kuongezeka


Watu wajiandikisha kutafuta ajira
Watu wajiandikisha kutafuta ajira

ILO inabashiria kuwa watu millioni 2.3 zaidi watapoteza ajira zao ifikapo mwisho wa mwaka huu .

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:48 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Shirika la kimataifa la kazi ILO linabashiri kuwa hali ya ukosefu wa ajira duniani itaendelea kuwa mbaya mnamo miaka 2 ijayo huku uchumi wa mataifa yanayoinukia na yanayoendelea utakua na mzigo mkubwa katika soko la ukosefu ajira. ILO imechapisha jana ripoti yake ya mwaka juu ya mwenendo wa soko la ajira kwa mwaka huu 2016 .

Shirika la ILO limegundua kuwa zaidi ya watu millioni 197 kote duniani hawakuwa na ajira mwishoni mwa mwaka jana, hiyo ikiwa ni millioni 27 zaidi kuliko idadi ya kabla ya mzozo wa ajira hapo mwaka 2007.

ILO inabashiria kuwa watu millioni 2.3 zaidi watapoteza ajira zao ifikapo mwisho wa mwaka huu kukiwa na wengine millioni 1.1 zaidi hapo mwaka 2017, na hiyo kufikisha idadi ya watu wasiokua na ajira kuwa millioni mia 2.5.

Mkurugenzi mkuu wa ILO, Guy Ryder, anasema ukuwaji wa polepole wa uchumi wa dunia haubuni nafasi za ajira za kutosha kubadili hali inayoongezeka ya idadi kubwa ya ukosefu wa ajira duniani.

Bw. Ryder anasema, idadi hizi zinaonyesha kudorora kwa hali ya ukosefu wa ajira, hususan katika dunia inayoimarika kiuchumi na mataifa yanayoendelea na kuna kiwango kidogo cha kuimarika anaweza kusema katika nchi ziloendelea kiviwanda. Lakini kuimarika huko haitatosha bila shaka kusawazisha kupunguwa kwa ajira unaoonekaa hususan katika nchi zenye uchumi unaoinukia.

Bw Ryder anasema hali hio itaendelea kusababisha ukosefu wa ajira katika siku za usoni. Alitaja Brazil, China na mataifa yanayozalisha mafuta kwa kuwa nchi ziloathiriwa zaidi na kudhoifika kwa soko ya ajira.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba changamoto inayobaki ni kupata ajira nzuri. Wakati viwango vya umasikini vimepunguwa, ILO inaeleza kiwango cha kushuka katika idadi ya wafanyakazi masikini katika nchi zinazoendelea imedorora. ILO inaeleza, takriban watu billioni 1.5 wanafanyakazi katika soko lililodhaifu.

Hii inajumlisha watu ambao wanajiajiri wenyewe au wanafanyakazi katika sekta isiyo rasmi. Ni ajira zenye uzalishaji mdogo, na mshahara mdogo na haina usalama wowote wa kijamii. Inagundua nchi kama vile Kusini mwa Asia na nchi kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika kuwa na viwango vikubwa vya ajira dhaifu, zikiwa katika asli mia 74 kusini mwa Asia na asli mia 70 katika nchi kusini mwa jangwa la sahara.

Waandishi wa ripoti hiyo wanasema, serikali zinapaswa kuimarisha sera za ajira, na kuweka mifumo ya usalama wa kijamii, na kukabiliana na hali mbaya ya kutokuwa na usawa. Wanasema lazima kipaumbele zaidi kiwekwe katika kusaidia watu ambao wanakumbwa na hali ngumu ya kuingia katika soko ya ajira . Hii inajumlisha vijana, wanawake, wale ambao wamkaa mda mrefu bila kuwa na ajira na walemavu.

XS
SM
MD
LG