Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:33

UN yasema wanawake 131 walibakwa Sudan Kusini ndani ya kipindi cha miezi tatu


Wanawake wa Sudan Kusini wakipanga foleni ili kupata chakula
Wanawake wa Sudan Kusini wakipanga foleni ili kupata chakula

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini ,UNMISS pamoja na ofisi ya Umoja wa mataifa ya haki za binadamu wamesema kwamba takriban wanawake 131 na wasichana walibakwa.

Ripoti hiyo inaongeza kusema kwamba karibu raia 200 wameuwawa kwenye jimbo lililotatizika la Unity, katika muda wa miezi mitatu. Mashirika hayo mawili yameorodhesha ukiukwaji wa haki za kimataifa za binadamu pamoja na sheria za kimataifa za haki za binadamu kwenye jimbo la Unity nchini humo. Ukatili huo unasemekana kutokea wakati wa mapigano kati ya vikosi vya serikali vikishirikiana na makundi rafiki yenye silaha, dhidi ya vile vya SPLM/IO ambavyo ni vitiifu kwa makamu wa rais Riek Machar.

UNMISS imesema kwamba ripoti hiyo inaangazia kati ya Februari 11 na Mei 31 mwaka huu kwenye kaunti 3 za jimbo la Unity za Koch, Leer na Mayendit. UNMISS ilisema Aprili kwamba takriban watu 72 waliuwawa Sudan kusini, huku wasichana 64 pamoja na wanawake wakibakwa kati ya Februari na Aprili kwenye kaunti ya Leer kwenye jimbo la Unity.

XS
SM
MD
LG