Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:43

UN yasema takriban watu 440 waliuwawa Sudan Kusini mwaka jana


Mtu akijiandaa kuchukua miili ya watu waliyokufa kwa ajili ya mazishi kwenye eneo la Yei , Sudan Kusini, kwenye picha ya maktaba.
Mtu akijiandaa kuchukua miili ya watu waliyokufa kwa ajili ya mazishi kwenye eneo la Yei , Sudan Kusini, kwenye picha ya maktaba.

Umoja wa Mataifa umesema Jumanne kwamba takriban watu 440 walikufa kutokana na mapigano mabaya kwenye jimbo la Western Equatoria nchini Sudan kusini ndani ya kipindi cha miezi michache mwaka uliopita.

Taarifa hiyo imetolewa muda mfupi baada ya Umoja huo kutoa ripoti nyingine mwezi uliopita ikionya kwamba taifa hilo changa zaidi duniani huenda likatumbukia tena kwenye mapigano, wakati ghasia za kikabila pamoja na migogoro ya kisiasa zikiendelea kuongezeka.

Kulingana na ripoti ya pamoja ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, na ofisi ya haki ya kibinadamu, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na mauaji unafanyika katika wilaya ya Tambura katika jimbo la Western Equatoria,.

Ripoti hiyo inawalaumu kwa pamoja wanajeshi watiifu kwa rais Salva Kiir na wapiganaji wa kundi la SPLM/A-IO wanao ongozwa na makamu wa rais Riek Machar pamoja na washirika wa pande zote mbili. Ripoti inaeleza kwamba mbali na rais 440 walouliwa kati ya June na Septemba mwaka jana katika wilaya ya Tambura kuna visa 64 vya ubakaji vilivyoripotiwa na watu 74 kutekwa nyara.

XS
SM
MD
LG