Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 08, 2024 Local time: 16:22

UN yaelezea wasi wasi wake kuhusu uchaguzi wa Venezuela


Mgombea urais wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado akivalia mavazi ya kitamaduni kwenye mkutano wa kampeni. June 25, 2024.
Mgombea urais wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado akivalia mavazi ya kitamaduni kwenye mkutano wa kampeni. June 25, 2024.

Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Turk, ameonya kuwa uchaguzi ujao wa rais nchini Venezuela, huenda usiwe huru na wa  haki kutokana na ukandamizaji uliotanda kote nchini, ukizuia sauti za wananchi kusikika.

Kwenye taarifa za karibuni zaidi kuhusu haki za binadamu nchini humo, Turk ameelezea kuhusu serikali ya kiimla, inayowakandamiza wapinzani wake, kwa kuwakamata pamoja na kuwateka nyara.

“Ofisi yangu inaendelea kupokea ripoti za ukamataji kuelekea siku ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa wafuasi na wanachama wa upinzani. "Hili halikai vizuri na ningeomba liachwe,” amesema Turk, wakati akiwa katika kikao na baraza la haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Jumatano na Alhamisi.

Ofisi yake imeorodhesha kwa wasi wasi mkubwa, ongezeko la vitisho, ukandamizaji na mashambulizi dhidi ya asasi za kiraia, wanahabari, viongozi wa vyama vya wafanyakazi, pamoja na sauti nyingine zinazochukuliwa kuikosoa serikali.

Hayo yanafanyika kupitia ukamataji na kufunguliwa mashtaka pamoja na kesi 38 za ukamataji holela. Januari serikali ilimuondoa mmoja wa wapinzani wakuu wa rais Nicholas Maduro, Maria Corina Machado, kwa kumpiga marufuku kuwania urais kwa miaka 15.

Mwezi Aprili muungano wa vyama vya upinzani ulikubaliana kumuunga mkono Edmund Gonzalez dhidi ya Maduro, uamuzi ambao waangalizi wanasema huenda ukaleta ushindi.

Forum

XS
SM
MD
LG