Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 02, 2024 Local time: 01:08

UN kuongeza muda kwa kikosi cha kulinda amani Haiti


Maafisa wa polisi wa Kenya wakipiga doria kwenye mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, Julai 17, 2024.
Maafisa wa polisi wa Kenya wakipiga doria kwenye mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, Julai 17, 2024.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu limeidhinisha kuongeza muda wa mwaka mmoja zaidi kwa kikosi cha kimataifa cha polisi nchini Haiti kinachosaidiana na polisi wa kitaifa  kukabiliana na magenge.

Hitua hiyo inalenga kusaidia taifa hilo la Caribbean lililogubikwa na ghasia, wakati baraza hilo likitathmini kuweka operesheni kamili ya walinda amani wa UN nchini humo.

"Wakati wa kupitisha azimio hili hivi leo, baraza liliisaidia Haiti kuendelea kuweka tena usalama na kuunda mazingira muhimu ya kuitisha uchaguzi huru na wa haki,” balozi wa Marekani Linda Thoma-Greenfield alisema, “ Kwa hiyo tufanye kazi pamoja kujenga kwa maendeleo ya Kikosi cha Kimataifa cha Usalama MSS kwa ajili Haiti." Tukumbatie mwelekeo mpya ambao ni endelevu. Tulinde fursa tete lakini zenye kutia hamasa ili kujenga mustakbali mzuri kwa watu wa Haiti.”

Marekani na Equador waliandika rasimu ya azimio ili kuongeza muda hadi Oktoba 2, 2025. Serikali ya mpito ya Haiti imeliomba Baraza la Usalama la UN lenye nchini wanachama 15, kuanza majadiliano kuelekea kuunda kikosi kilichopo, kuwa kikosi kamili cha walinda amani wa UN.

Kenya inaongoza kikosi cha polisi kilichoko Haiti,na Rais William Ruto kiasi cha wiki moja iliyopita aliitembelea Haiti na kuzungumza na maafisa wa polisi wa Kenya na Haiti. Kufikia sasa ni takriban polisi 500 ambao wamepelekwa nchini humo , wengi wao wakitokea Kenya. Wengine ni kutokea Jamaica na Belize. Wanadiplomasia wanatarajia kuwa nchi nyingine pia zitapeleka polisi nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG