Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 12:26

UN kubaki Libya hadi Januari


Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas akitoa hotuba kuhusiana na amani ya Libya kwenye picha ya awali.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas akitoa hotuba kuhusiana na amani ya Libya kwenye picha ya awali.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi limekubaliana kuendelea na shughuli za kisiasa nchini Libya hadi Januari 31, mwaka ujao. 

Wakati huo utakuwa muda mfupi baada ya taifa hilo kufanya uchaguzi wa rais. Baraza hilo lenye wanachama 15 limekuwa likishauriana kuhusu kuongeza jukumu lake la kisiasa nchini humo hadi Decemba 24 ambapo uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika.

Hata hivyo kulitokea mvutano mkali kati ya Uingereza na Russia kuhusiana na pendekezo hilo. Moscow ililamamikia lugha iliyokuwa kwenye rasimu ya mapendekezo, na ilioandikiwa London ikisema kwamba vikosi vya kigeni pamoja na mamluki nchini Libya waondoke pamoja na sehemu inayoeleza jukumu la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Jumatano Russia ilitishia kupinga pendekezo hilo lakini baadaye ikaamua kuongeza maandishi yake kwenye rasimu hiyo. Baada ya mkutano wa dharura kati ya wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo Alhamisi, makubaliano yalifikiwa ya kuongeza ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Libya hadi Januari 31. Wanachama hao ni Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Marekani.

XS
SM
MD
LG