Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 00:16

Umoja wa nchi za kiarabu umekataa pendekezo la kuhamisha wapalestina


Wapalestina wakitembea barabarani baada ya uharibifu wa nyumba zao kutokana na vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas
Wapalestina wakitembea barabarani baada ya uharibifu wa nyumba zao kutokana na vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas

Katibu mkuu wa umoja wa nchi za kiarabu Ahmed Aboul Gheit amekataa mpango wowote wa kuwahamisha wapalestina kutoka ukanda wa Gaza, akisema kwamba mpango kama huo hauwezi kukubalika.

Aboul Gheit ameambia mkutano wa viongozi wa serikali duniani kwamba pendekezo la rais wa Marekani Donald Trump kuwahamisha karibu wapalestina Milioni 2 kutoka Gaza, utapelekea kanda hiyo nzima kuingia katika mgogoro usiomalizika na kuvuruga amani na utulivu.

Gheit amesema hauwezi kukubalika kabisa na umoja wa nchi za kiarabu ambao umepigania kwa maslahi yake kwa miaka 100.

Baada ya mazungumzo na rais Trump, Mfalme wa Jordan Abdullah II amesema kwamba alisisitiza msimamo wa nchi yake wa kupinga kuondolewa kwa wapalestina kutoka Gaza na ukingo wa magharibi.

Amesema kwamba lengo kubwa ni kujenga upya Gaza bila kuwaondoa wapalestina, Pamoja na kuhsughulikia hali ya kibinadamu ambayo ni mbaya sana.

Amezungumzia pia kile ametaja kuwa mchango muhimu wa Trumo katika kuhakikisha kwamba vita vinamalizika Gaza na kutaka Marekani Pamoja na washirika wengine kuhakikisha kwamba mapigano yanakoma kabisa.

Forum

XS
SM
MD
LG