Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:24

Umoja wa Mataifa waomba msaada wa dola bilioni 2.6 kusaidia mamilioni ya waathirika wa njaa Somalia


Wasomalia waliotoroka maeneo yanayokumbwa na ukame wakipewa msaada wa chakula , kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani, kwenye vitongoji vya Mogadishu, Juni 30, 2022.
Wasomalia waliotoroka maeneo yanayokumbwa na ukame wakipewa msaada wa chakula , kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani, kwenye vitongoji vya Mogadishu, Juni 30, 2022.

Umoja wa mataifa unatoa wito wa msaada wa dola bilioni 2.6 mwaka huu kuwasaidia watu milioni 7.6 miongoni mwa Wasomali walio hatarini ambao wanakabiliwa na njaa kali na uwezekano wa njaa kutokana na mzozo, bei ghali ya chakula na hali ya ukame ambayo haijawahi kushuhudiwa .

“Kuna uwezekano mkubwa wa njaa kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu, na bila shaka baada ya kipindi hicho, ikiwa msaada wa kibinadamu hautaendelea kutolewa, na kama mvua za Aprili hadi Juni zitapungua kama inavyotabiriwa sasa,” Adam Abdelmoula, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Somalia amewaambia waandishi wa habari.

Nchi hiyo, pamoja na maeneo mengine ya Pembe ya Afrika, yanakabiliwa na ukame wa kihistoria baada ya uhaba wa mvua kwa misimu mitano mfululizo.

Abdelmoula amesema karibu watu milioni 6.4 wanakabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama wa chakula na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 8.3 kati ya mwezi Aprili na Juni, ikiwemo watu 727,000 kati ya hao ambao wanatarajiwa kukabiliwa na viwango vibaya vya njaa.

Umoja wa Mataifa unasema wale walio katika hatari kubwa wako katika wilaya za Baidoa na Burhakaba na miongoni mwa waliokimbia makazi yao katika mji wa Baidoa na katika mkoa wa Bay na mjini Mogadishu.

XS
SM
MD
LG