Balozi wa UAE nchini Iran, Saif Mohammed Al Zaabi, atarejea Teheran katika siku zijazo ili “kuendelea kusukuma mbele uhusiano wa pande mbili ili kufikia maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili jirani na eneo hilo, shirika la habari la serikali ya UAE WAM limeripoti.
Hatua hiyo inajiri huku wanadiplomasia wa Marekani na Iran wakitaka kumaliza mazungumzo ya miezi 16 kuhusu kufufua makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya Tehran pamoja na mataifa yenye nguvu duniani.
Wiki iliyopita, Kuwait ilimteua balozi wake mpya huko Teheran kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2016. Saudi Arabia imekuwa pia ikifanya juhudi kama hizo kwa kutuliza mvutano na Iran katika mfululizo wa mazungumzo ya upatanishi wa Baghdad.