Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 02, 2024 Local time: 22:27

UM wasema TTP ni kundi kubwa zaidi la kigaidi


Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP), muungano wa makundi yenye itikadi kali, ni kundi kubwa zaidi la kigaidi Afghanistan na linaungwa mkono zaidi na watawala wa Taliban kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka Pakistan.

Timu ya waangalizi wa vikwazo ya Umoja wa Mataifa ilitoa tathmini hiyo Jumatano usiku wakati kukiwa na ongezeko kubwa la mashambulizi ya kigaidi yanayoongozwa na TTP dhidi ya vikosi vya usalama vya Pakistani na raia, na kuua mamia yao katika wiki za hivi karibuni.

Ripoti imesema TTP inaendelea kufanyakazi kwa kiwango kikubwa Afghanistan kwa operesheni za kigaidi Pakistan kutoka huko, mara nyingi kwa kutumia Waafghani.

Ilibainisha kuwa kundi lililo tangazwa kimataifa kuwa la kigaidi na kujulikana pia kama Taliban wa Pakistani, linaendesha shughuli zake nchini Afghanistan likiwa na wastani wa wapiganaji kati ya 6,000 na 6,500.

Forum

XS
SM
MD
LG