Beasley amasema huenda hali hiyo ikashuhudiwa mwaka ujao iwapo Russia haitasitisha kuzuia usafrishaji wa chakula kutoka Ukraine, pamoja na kuuza mbolea yake kwenye masoko ya kimataifa. Beasley alikumbusha watu kuhusu mfumuko wa bei duniani wa mwaka 2008, ambapo bei ya za vya vyakula zilipanda sana, na kupelekea misukosuko pamoja na maandamano kwenye karibu mataifa 50 ulimwenguni.
Ameongeza kusema kwamba hali ya sasa ni mbaya zaidi, na tayari misukasiko imeanza kujitokeza kwenye baadhi ya mataifa kama vile Sri Lanka, Mali, Chad, Burkina Faso, Kenya, Pakistan, Peru na Indonesia miongoni mwa mengine. Kiongozi huyo amesema kwamba watu waliokuwa wakikabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula kabla ya uvamizi wa Russia walikua milioni 276, lakini sasa idadi inakisiwa kufika milioni 345.