Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:49

Wanaowania urais Kenya wapinga sharti la ukusanyaji saini


Maafisa wa IEBC akichukua alama za Vidole vya mpigaji kura wakati wa uandikishaji mapema mwaka huu.
Maafisa wa IEBC akichukua alama za Vidole vya mpigaji kura wakati wa uandikishaji mapema mwaka huu.

Mwaka huu kinyang’anyiro cha urais kinamsongamano. Tume ya uchaguzi (IEBC) imetangaza jumla ya wagombea 19, nane kati yao kutoka katika vyama vya siasa na 11 ni wagombea binafsi.

Mbali na wagombea wawili maarufu- Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga- kuna wagombea 17 wengine ambao wamelalamika kwa hasira kubwa kwa habari zao kutotangazwa vyakutosha na vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, hivi karibuni IEBC iliwakatisha tamaa wagombea binafsi ilipotangaza kuwa wanatakiwa kupata sahihi 48,000, angalau 2,000 kutoka katika kaunti 24 na ziwe za wale wanaowaunga mkono ambao hawako katika chama chochote.

Masharti haya mapya yamekosolewa sana na baadhi ya hao wagombea binafsi wanaodai kuwa IEBC inawawekea mtego na inawazuia bila ya haki yoyote kushiriki katika mbio za urais.

Baadhi ya wagombea binafsi kama vile Nazlin Umar wameapa kupinga mashartihayo mapya na kupigania haki yao mahakamani.

Orodha ya wagombea “wengine” wa urais ni mchanganyiko wa magwiji wa siasa na wagombea wapya, maprofesa na mshauri wa zamani wa rais, mawakili na waalimu, pamoja na baadhi ya majina ambayo Wakenya wanayasikia kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari ilikuwa sio rahisi kuja na wasifu wa orodha kamili ya wagombea urais wengine 17, kwa hivyo hapa kuna orodha ya wagombea watano waliokuwa na mvuto zaidi.

Mohammed Abduba Dida

Dida, ana umri wa miaka 43, aliyepata umaarufu mwaka 2013 alipogombea nafasi ya urais kwa tiketi ya chama cha Alliance of Real Change.

Aliwahi kuwamwalimu wa kiingereza na fasihi katika shule ya Lenana High School aliyewashitua watu wengi alipopata jumla ya kura 52,848, na kufikia kuwa gwiji la siasa kama vile Martha Karua.

Hivi sasa amerudi kwenye ulingo wa siasa na anawaomba Wakenya kupuuza kura za ukabila na kuacha “kuwategemea wale waliofeli katika uongozi”.

****

Nazlin Umar Fazaldin Rajput

Iwapo Nazlin Umar atakuwa rais hivi leo, basi mwanamke huyu atakuwa ameandika historia kwa namna mbili.

Kwanza kama mwanamke wa kwanza kuwa rais, na pili ni Muislam wa kwanza kuwa rais.

Anapingana na mtu yoyote ambaye anawashutumu Wakenya kwa ukabila na badala yake anasema Wakenya ni wahanga wa wanasiasa waliobobea kwenye ukabila ambao wameingiza upotoshaji wa dhana yote ya ufahamu wa ukabila.

****

Dr Ekuru Aukot
Huyu ni mmoja wa wanasheria ambao Wakenya hawana budi kuwashukuru kwa kuweza kuiandika katiba ya Kenya (2010).

Mtu huyu anatokea kijiji chaKapedo katika kaunti ya Turkana na ni kati ya wale watu wa kwanza ambao walitangaza nia ya kugombea urais March 2016 kupitia chama cha Thirdway Alliance.

Pia ni mtoto wa mzee Aukot Tarkus na anatokea katika familia yenye mitala na watoto 27. Anataka kutokomeza tatizo la ufisadi.

****

Joe Nyagah

Wiki hii, Joe Nyagah alianzisha juhudi zake za kugombea urais na kutangaza kwamba tayari amevuka kikwazo cha saini 48,000 kwani tayari ana saini 60,000, 2,000 kati ya hizo kutoka katika kaunti 30.

Nyagah, alijiuzulu kama mshauri wa rais katika masuala ya ushirikiano wa kimaeneo na ni Chancela wa chuo cha ushirika, akisema amechoshwa na vita vya ndani kati ya viongozi wa juu wa Jubilee.

Nyagah alizaliwa mwaka 1948, na mwanasiasa mkongwe.

****

Muthiora Kariara

Ni mwenye umri wa miaka 35 na alikuwa ni mfanyakazi wa Benki iitwayo Consolidated Bank ambaye ndoto yake ni “ni kuunganisha makabila” katika taifa la Kenya na ameahidi kuwaunganisha Wakenya kwa njia yoyote ile”.

Pia ameahidi “kutovumilia” ufisadi na ameahidi kuwafunga jela wale wenye kupandikiza chuki.

XS
SM
MD
LG