Makubaliano hayo yalikuja wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alipoitembelea Brussels katika safari ambayo pia inajumuisha kwenda Uhispania na Ureno kutafuta msaada mpya wa kupambana na uvamizi wa Russia ulioanza mapema mwaka 2022.
Makubaliano hayo yanahakikisha msaada wa usalama wa Ubelgiji kwa wakati unaofaa, magari ya kisasa ya kivita, vifaa vya kukidhi mahitaji ya jeshi la anga na ulinzi wa anga wa Ukraine, usalama wa majini, kuondoa mabomu ya kutegwa ardhini, ushiriki katika muungano wa silaha za kivita, na mafunzo ya kijeshi, Zelenskyy alisema kwenye mtandao wa X.
Kiongozi huyo wa Ukraine alisema makubaliano hayo ya miaka 10 pia yanajumuisha kushirikiana na Ubelgiji katika masuala ya kijasusi, usalama wa mtandao, kukabiliana na taarifa potofu na sekta ya ulinzi.
Forum