Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 10:01

Ukraine yahifadhi ushahidi kuhusiana na kunyongwa kwa wafungwa 93 wa vita

Mama Kateryna na familia yake wakilia juu ya jeneza la mtoto wake Ihor Kusochek, askari wa Kiukreni wa kikosi cha Azov ambaye aliuwawa kwenye mstari wa mbele huko Toretsk, katika mkoa wa Chernihiv, Ukraine, Ijumaa Oktoba 4, 2024. (AP).

Ukraine imehifadhi ushahidi kuhusiana na kunyongwa kwa wafungwa 93 wa vita wa Ukraine kwa mujibu  wa afisa wa sheria aliyepewa jukumu la kuchunguza uhalifu wa kivita

Ukraine imehifadhi ushahidi kuhusiana na kunyongwa kwa wafungwa 93 wa vita wa Ukraine kwa mujibu wa afisa wa sheria aliyepewa jukumu la kuchunguza uhalifu wa kivita unaohusiana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Yuriy Belousov ambaye anaongoza idara ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu anayehusika na uchunguzi wa uhalifu uliofanywa katika vita vya kutumia silaha alitoa takwimu ya hivi karibuni wakati alipozungumza na vyombo vya habari moja kwa moja siku ya Ijumaa.

"Sasa tuna habari kuhusu vifo vya wanajeshi wetu 93 ambao waliuwawa kwenye uwanja wa vita" Belousov aliiambia Yedyniy Novyny, matangazo ambayo yanaunganisha chaneli nyingi za televisheni za Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG