Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:06

Ukraine yaelezwa kufanya oparesheni zaidi katika maeneo makuu matatu


Wizara ya ulinzi ya Uingereza, Jumapili katika ripoti yake ya kila siku ya kijasusi kuhusu Ukraine, imesema kwamba katika siku za hivi karibuni, Ukraine imefanya tena operesheni kubwa kwenye maeneo makuu matatu kusini na mashariki mwa Ukraine.

Katika ripoti hiyo iliyotumwa kwenye Twitter, imesema wanajeshi wa Ukraine wamejifunza kutokana na uzoefu wao katika wiki mbili za kwanza za mashambulizi hayo na kuboresha mbinu za kushambulia ulinzi wa kina wa Russia, ulioandaliwa vyema.

Wanajeshi wa Ukraine wamesonga mbele kuelekea pande kadhaa kuzunguka mji wa Bakhmut katika mkoa wa Donetsk, naibu waziri wa ulinzi Hanna Maliar, amesema Jumamosi.

“Kuna maendeleo katika pande zote,” aliandika kwenye Telegraph.

Maliar alisema kuwa maendeleo hayo yamefanyika karibu na vijiji vya Orikhovo - Vasylivka, Bohdanivka, Yahidne, Klishchiivka, na Kurdyumivka na kuongeza kuwa mapigano yanaendelea kusini mwa nchi.

Forum

XS
SM
MD
LG