Droni hizo aina ya Shahed zilizotengenezewa iran ziliangushwa katika mkoa wa kati wa Poltava, mkoa wa kusini mashariki wa Zaporizhzhia na Dnipropetrovsk, pamoja na Kharkiv upande wa kaskazini, taarifa imeongeza kusema.
Kombora moja la Russia aina ya X-59 lililorushwa kutoka mkoa wa Kursk ndani ya Russia pia lilitunguliwa. Gavana wa mkoa wa Dnipropetrovsk, Serjiy Lysak amesema kuwa mashambulizi ya droni ya usiku kucha yameharibu majengo ya biashara na makazi, pamoja na nyaya za umeme.
Wakati huo huo vitengo vya ulinzi wa anga vya Russia mapema leo, vimeharibu ndege tatu zisizo na rubani za Ukraine kwenye mji wa Russia wa Mozdok, kwenye mkoa wa Ossetia Alania Kusini, mkuu wake Sergey Meniaylo amesema, likiwa shambulizi la kwanza kwenye eneo hilo kulingana na Russia.
Meniaylo ameongeza kusema kuwa shambulizi hilo lilikuwa limelenga uwanja wa ndege wa kijeshi.
Forum