Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 02:03

Ukraine na Russia zashutumiana kwa ugaidi huku makombora zaidi yakirushwa nchini Ukraine


Meli ya vita ya Russia kwa jina Aleksin ikifyatua makombora kutoka baharini wakati wa gwaride la kijeshi kuadimisha siku ya wanajeshi wa majini katika eneo la Kaliningrad, Russia, July 31, 2022
Meli ya vita ya Russia kwa jina Aleksin ikifyatua makombora kutoka baharini wakati wa gwaride la kijeshi kuadimisha siku ya wanajeshi wa majini katika eneo la Kaliningrad, Russia, July 31, 2022

Msururu mwingine wa makombora ya Russia umeangushwa katika mji wa Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine, huku idadi ya vifo kutokana na shambulizi la makombora yaliyoangushwa na Russia jumatatu, ikifikia 19.

Makombora yamepiga shule, kituo cha afya na nyumba za watu katika mji wa Zaporizhzhia.

Makombora ya masafa marefu aina ya 12 S-300 yamepiga majengo ya serikali na kusababisha moto mkubwa katika sehemu hiyo, mtu mmoja amethibitishwa kufariki katika shambulizi la Jumanne.

Shambulizi hilo limetokea asubuhi.

Huduma ya dharura nchini Ukraine imesema kwamba watu 19 wamefariki na wengine 105 kujeruhiwa katika shambulizi la Jumatatu.

Makombora ya Russia yaliharibu mifumo muhimu mjini Kyiv na katika maeneo mengine 12.

Zaidi ya miji 300 ilikosa umeme, ikiwemo sehemu za mji wa Kyiv na Lviv, mpakani na Poland.

Wanajeshi wa Ukraine wameendelea kuwazidi nguvu wa Russia

Magari ya jeshi la Russia yaliyoachwa baada ya wanajeshi wa Russia kukimbia katika eneo la Kharkiv, Sept 11, 2022
Magari ya jeshi la Russia yaliyoachwa baada ya wanajeshi wa Russia kukimbia katika eneo la Kharkiv, Sept 11, 2022

Wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kupambana na wanajeshi wa Russia na wamefanikiwa kuwaruisha nyuma wanajeshi wa Russia.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Ryabkov, ameonya kwamba misaada ya nchi za mgaharibi kwa Ukraine, ikiwemo kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine katika nchi wanachama wa NATO, na kutoa taarifa za ujasusi kwa wanajeshi wa Ukraine kuhusu sehemu ambazo Russia inalenga, ni dhihirisho kwamba mataifa ya Magharibi yanahusika moja kwa moja na vita vya Ukraine na kuusaidia utawala wa Kyiv.

Ryabkov amesema kwamba “Russia italazimika kuchukua hatua za kujibu zikiwemo zile zinazofanana kabisa.” Akiongezea kwamba “japo Russia haina nia ya kujiingiza katika mgongano wa moja kwa moja na Marekani pamoja na NATO, tuna matumaini kwamba Washington na nchi nyingine za Magharibi zinajua hatari iliyopo ya vita kuendelea bila kudhibitiwa.”

Russia na Belarus zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja

Mwanajeshi wa Russia (Kulia) akiwa na mwenzake wa Belarus wakati wa mazoezi ya pamoja Februari 19,2022
Mwanajeshi wa Russia (Kulia) akiwa na mwenzake wa Belarus wakati wa mazoezi ya pamoja Februari 19,2022

Onyo la Ryabkov linajiri baada ya rais wa Belarus Alexander Lukashenko kutangaza kwamba amekubaliana na rais wa Russia Vladimir Putin kuunda jeshi la pamoja kukabiliana na kile Lukashenko amedai kuwa “uwezekano wa Ukraine kuishambulia Belarus.”

Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema kwamba hajaona “ushahidi wa wanajeshi kujikusanya nchini Belarus kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi,” lakini ameonya kwamba “huenda Russia ikaendelea kumshambulia majirani yake bila kuchokozwa, na kuharibu mifumo muhimu ya Ukraine kwa kutumia makombora ya masafa marefu.”

“Adui hataacha kuzishambulia Khartiv na Kherson. Anajaribu kutishia watu wa Ukraine na kusababisha hofu.” Amesema mkuu wa jeshi la Ukraine.

Taasisi ya kuchunguza vita yenye makao yake mjini Washington, imesema kwamba hakuna ishara kwamba jeshi la pamoja kati ya Belarus na Russia litatekeleza shambulizi dhidi ya Ukraine kutoka sehemu za kaskazini.

Putin ameapa kuendelea kuangusha makombora Ukraine

Japo maafisa wa Ukraine wamesema kwamba makombora ya Russia yaliyoangushwa Jumatatu hayakuwa na maana yoyote ya kijeshi, Putin amesema kwamba “shambulizi hilo lilikuwa jibu la shambulizi lililopelekea uharibifu kwenye daraja muhimu linalounganisha Crimea na Russia,” na kudai kwamba shambulizi kwenye daraja lilipangwa na wanajeshi maalum wa Ukraine.

Daraja linalounganisha Russia na Crimea likiwaka moto kutokana na shambulizi la Oct 8 2022.
Daraja linalounganisha Russia na Crimea likiwaka moto kutokana na shambulizi la Oct 8 2022.

Putin ameapa kwamba atajibu “kwa nguvu zinazostahili” iwapo Ukraine itaendelea kutishia usalama wa Russia.

“Hakuna yeyote anastahili kuwa na shaka na hilo,” ameliambia baraza la uslama la Russia kwa njia ya video.

Putina amelitaja shambulizi dhidi ya daraja kuwa “kitendo cha kigaidi.”

Spika wa bunge la Russia amemlinganisha rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaida, Osama bin Laden.

Amesema kwamba “kuiunga mkono Ukraine ni sawa na kufadhili ugaidi,” na kwamba “mazungumzo hayawezi kufanyika na magaidi.”

Zelenskyy amewataka viongozi duniani kutangaza Russia kuwa nchi ya kigaidi kutokana na hatua yake ya kushambulia raia na kutekeleza uhalifu wa kivita.

XS
SM
MD
LG