Maafisa wa Ukraine, Jumapili wameanzisha uchunguzi wa shutuma kwamba vikosi vya Russia vimewauwa wanajeshi wa Ukraine waliojisalimisha.
Hiyo ni baada ya kusambaa video katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha wanaume wawili wasiokuwa na sare za kijeshi wakifyatuliwa risasi kwa karibu baada ya kutoka mafichoni.
Ofisi ya mwendesha mashitaka imesema kupitia Telegram, Jumapili kwamba video zimeonyesha kundi la wanajeshi wa Russia wakifyatua risasi kwa karibu kwa wanajeshi wawili wasio na silaha wala sare ambao walijisalimisha.
Video ilionekana Jumamosi, katika mtandao wa DeepState, wa Ukraine ambao unaripoti masuala ya vita. Inaonyesha wanajeshi walio jisalimisha mmoja wao akinyoosha mikono juu akitoka nje akiwa amewekewa wa bunduki, na kulala chini kabla ya kundi la wanajeshi wa Russia kuanza kumfyatulia risasi. Hakuna majibu yoyote kutoka Russia kuhusiana na tukio hilo.
Forum